Users Online : 3

SIRI YA PADRE NA MKE WANGU SEHEMU YA 1 (Sikiliza au shuka chini kuisoma)

Scroll chini ya audio Imesimuliwa kwa maandishi,pia kila Tarehe moja tunatoa simulizi mpya sauti na maandishi

    
  

NDOA YANGU!


MTUNZI: McLAURIAN


WASAP: 0768276551


PART: 1.


Ndoa yangu jamani ndoa yanguu....

Kama ilivyo kawaida kwa mwanadamu baada ya kufikisha miaka fulani, hutakiwa kuwa na mwenza wake na hatimaye huweza kufunga ndoa na kuwa mme na mke.

Mungu akijalia huweza kupata mtoto au watoto.


Ilikuwa baada ya kujiunga na kwaya ambayo sitoitaja katika parokia inayopatikana mkoani Tabora.

Nilikuwa hodari sana wa kupiga kinanda lakini pia fundi wa kufundisha nyimbo pamoja na kuongoza wana kwaya wenzangu.


Ilitokea mpaka nikawa nimependwa sana na baba paroko wa parokia hiyo kutokana na ufundi wangu.

Miongoni mwa wanakwaya niliokuwa nawaongoza alikuwemo binti mmoja mzuri kwelikweli aliyekuwa anavaa kiheshima.

Nilianza kumfatilia kwa chinichini ili kuweza kupata taarifa zake kwa ufasaha.


Zoezi hilo nililifanya kwa takribani miezi 2 ndipo nilipojiridhisha kuwa anatabia nzuri na anafaa kuwa mke wangu.

Kwa kuwa nilikuwa kiongozi, nilipata wakati mgumu sana wa kumtokea binti huyo aliyekuwa mzuri kwelikweli.

Siku moja niliamua kuvaa suti kisha nikajipitisha mbele yake na siku hiyo nilienda kuongoza kwaya ili nionekane vizuri.


Baada ya ibada kama bahati fulani, binti huyo ambaye jina lake ni Rose alinifuata na kunipa mkono kisha akanipongeza kwa ufundi niliouonesha. Nilifurahi sana kisha nikacheka. Baada ya hapo nilitamani kumwambia kuwa ninampenda lakini nilishindwa kutokana na aibu zangu.

Nilienda kwenye ofisi ya katekista kisha nikatoa bahasha moja na kwa ndani nikaandika ujumbe wa kumtaka Rose nifunge naye ndoa.


Baada ya kutoka pale ofisini, niliongezea kiasi cha sh 20 kisha nikaifunga na kumwambia kuwa hii bahasha nimepewa na Katekista hivo uisome lakini ukiwa peke yako.

Alicheka sana kisha akaiweka kwenye mkoba wake kwani tulikuwa kwenye watu wengi.

Tuliagana kisha tukaondoka, nilipofika nyumbani roho ikaanza kunicheza na kuwaza kuwa itakuwaje kama atanikataa wakati mimi ndiye kiongozi wake?.


Kesho yake ilikuwa siku ya kufanya mazoezi na mimi ndiye niliyekuwa mwalimu wao. Niliwahi kwa ajili ya maandalizi.

Gafla nilimuona Rose huku akionekana kunikwepa fulani, nami nikaogopa nikajisemea kuwa hapo nimeharibu kabisa.


Tulianza mazoezi huku nikiwa naogopa sana kuangaliana naye usoni.

Maisha yaliendelea hivohivo kwa mda huku tukiwa hatujaongea chochote baada ya kumpa bahasha ile.

Kwa kuwa nilikuwa na mahusiano mazuri na Baba paroko, nilijitoa muhanga na kisha nikaongea naye kuwa ninataka kufunga ndoa takatifu na Rose lakini nashindwa nianzie wapi.


Baba paroko, alinipongeza kwa hatua hiyo na kunambia kuwa atatukutanisha siku ya kesho baada ya mazoezi ya kwaya 

Nilishukuru kisha nikaondoka.

Kesho yake tulienda kwa Baba  paroko kisha  akatuelezea mambo mengi na hatua ambazo tunapaswa kufuata.

Rose alionekana kufurahia kisha wote tukapeana mikono.

Miongoni mwa vitu alivyotukataza ni kufanya mapenzi kabla hatujafunga ndoa.


Alitwambia kuwa kuanzia wiki iliyokuwa inafuata kuanza mafunzo ya uchumba na ndoa.

Tulianza mafunzo hayo kwa pamoja kisha tukawa tunarudi nyumbani kwa pamoja.


Siku moja tulienda kwenye mafunzo na kisha akasema kuwa tusubiri badae, na baada ya mda alinambia kuwa ninaweza kuondoka kwani mafunzo ya siku ile yalimuhusu Rose tu.

Baada ya kauli hiyo niliondoka nikamuacha Rose.

Kilichoendelea wala sikujua.

Mafunzo yaliendelea lakini siku moja nikajiuliza kwa nini mimi sijawahi bakizwa? .


Nilikosa jibu lakini nikawa na hofu fulani.

Rose alipewa  nafasi ya kuwa anawasaidia watoto yatima kwa kuongozana na Baba Paroko katika sehemu mbalimbali.

Alianza kumsifia kwelikweli mpaka waumini wakawa wanampigia makofi.


Nilianza kuhisi kitu maana Rose ukaribu wangu kwake ulianza kupungua na kuanza kuonekana mtu mkubwa sana.

Badae tuliandikisha Tangazo la ndoa na kisha tukaanza kutangazwa kanisani.


Rose ngozi yake ilianza kuwa nyororo kwelikweli. Baada ya tangazo hilo, habari za chinichini zilianza kusikika miongoni mwa Wanakwaya kuwa Rose anatembea na Baba Paroko.


Sikuweza kuzitilia maanani kwani nilijua kuwa ni mpango ambao wanaufanya ili kuweza kuharibu ndoa yetu isifanikiwe.

Rose wakati ule, alianza kuwa mzoefu wa Parokia mpaka siku moja mwenyekiti wa Parokia alitangaza kuwa wanawake na mabinti waache kwenda kwenye nyumba za mapadre kwani kule sio ofisi na utaratibu uko wazi kabisa.


Waumini wote kanisani walicheka kwelikweli.

Waswahili husema kuwa lisemwalo lipo na kama halipo laja .

Siku moja bwana baada ya mafunzo ambayo yalikuwa yanafanyika jioni, Katekista aliniita na kunambia kuwa utaratibu wa mafunzo mnapaswa kuwa wote kwa pamoja. 


Hakuishia hapo tu bali aliniambia kuwa ndoa yangu hii itakuwa na changamoto kwani mwenendo wa Rose ameshaustukia.

Aliishia hapo wala hakutaka kuongeza neno lolote kisha akanambia uamuzi ni wangu.


Kichwa kilianza kuuma, mbona Rose ni mtu wa kanisa? mbona Rose hajawahi vaa nguo fupi? mbona Rose hanywi pombe lakini pia ni mwanakwaya?.

Hayo ni maswali ambayo nilijiuliza.

Mda wa kufunga ndoa ulikaribia na tukawa tumebakiza wiki moja na kwa kuwa Paroko alishasema sio lazima sherehe sikuwaza kuhusu hilo.

Kiukweli Rose ni mzuri na laiti angevaa nguo fupi na kupaka makeup mmmhh  sijui..


Baada ya kubakia siku 3 kabla ya ndoa, Baba Paroko alituita tena na kisha tukapata mafunzo kisha akanambia kuwa ninaweza kuondoka lakini alimtaka Rose kubaki kwa Mazungumzo ya jinsi ya kuinua jumuiya za akina mama.


Nilitoka nje ikiwa ni mida ya saa 12 na nusu jioni.

Roho yangu siku hiyo ilihisi kitu fulani mpaka hatua nilizokuwa nataka kwenda nyumbani, nikawa nimeshindwa.

Nilisogea kidogo mpaka pembeni ya kanisa nikapumzika kwanza.

JE NINI KILIJIRI?...

PART 2

 NDOA YANGU

MTUNZI: McLAURIAN

WASAP: 0768276551

PART: 02

Ilipoishia, baada ya kubakia siku 3 kabla ya ndoa, Baba Paroko alituita tena na kisha tukapata mafunzo kisha akanambia kuwa ninaweza kuondoka lakini alimtaka Rose kubaki kwa Mazungumzo ya jinsi ya kuinua jumuiya za akina mama.

Nilitoka nje ikiwa ni mida ya saa 12 na nusu jioni.

Roho yangu siku hiyo ilihisi kitu fulani mpaka hatua nilizokuwa nataka kwenda nyumbani, nikawa nimeshindwa.

Nilisogea kidogo mpaka pembeni ya kanisa nikapumzika kwanza.


SONGA NAYO...

Niliendelea kukaa nje mpaka giza likaanza kuingia sasa huku huku nikiwa naangaza kila kona ili kuona kama Rose ameshatoka kwa Baba Paroko.

Maeneo yale yalikuwa na miti mingi kwelikweli ndipo mbu walipoanza kunishambulia kama siafu.

Nilitamani kuondoka lakini kwa kuwa nilikaa mda mrefu niliona busara kubaki ili niweze kuondoka naye.

Mda uliendelea kutaradadi kabisa na baada ya kuangalia saa yangu, nilikuta tiyari ni saa mbili kamili usiku.

Nilianza kujiuliza maswali kuwa kwa nini hatokei?

Nikiwa nimekaa, gafla niliona gari  aina ya pickup  linatoka kwenye geti la nyumba ya Paroko.

Kwa kuwa alikuwa ashanambia niondoke, nilijibaba ukutani kwani mwanga wa gari ungeweza kunimulika na kusababisga kuonekana.

Nikiwa nimejibanza, gafla kwa nyuma yangu nilisikia kama mtu fulani hivi, niligeuka na kukuta ni Sister

Niliishiwa ujanja lakini kwa sababu nilikuwa ninafahamika kanisani, hata sister yule aliyekuwa anatwa Gaudioza hakusita kunijua.

Nilimsogelea kisha nikampa salamu  kisha akaniuliza kuwa,


 

      "Kwanini upo hapa mda huu"?


Nilimjibu kuwa kuna mtu nimemsubiria ili niondoke naye.

Aliendelea kunihojihoji kisha nikamwambia kuwa ni mchumba wangu Rose ambaye nimemuacha ofisini na Paroko.


Sister aliguna kidogo kisha akawa ameniambia nimsindikize kwa Paroko kwani alikuwa na shida naye kama alivyodai.

Sasa niliona mtihani mkubwa kuongozana naye kwani angehisi kuwa namchora nami sikutaka kuonekana hivo kwani tulikuwa tunaheshimiana kweli.


Wakati bado nimesimama na Sister Gaudioza, pickup ile ikaanga kuunguruma huku ikionekana kupita sehemu tuliyokuwa tumesimama.


Baada ya kuona hivo, aliniambia kuwa tumsubiri hapo tulipokuwa kwani mwendo wake ulikuwa sio wa kasi.

Bila kuchelewa, Sister Gaudioza, alimpungia mkono Baba Paroko kisha akasimamisha gari .


Kuja kuangalia, nilimuona Rose akiwa amekaa kwenye gari hiyo na  baada ya mboni yangu kuangaliana na yake, aliinama kisha akajifanya anapiga chafya.

Wakati naangalia hivo, baba Paroko alinipungia mkono kisha akaniuliza,


" Mtumishi,...bado ulikuwa hujaenda nyumbani"?.


Nilimjibu kuwa, niliamua kumsubiri Rose kwa kuwa kuna giza ili niende naye.

Paroko mara baada ya kusikia hivo, alinambia kuwa, Kuna mgonjwa amezidiwa hivo Rose anaondoka naye na akitoka atampeleka mpaka nyumbani kwao.


Sikuwa na la kuongeza, kisha akawasha gari nakuondoka.

Baada ya kuondoka, Sister Gaudioza, alinambia nimsindikize mpaka nyumbani kwake kwani alikuwa haoni vizuri.

Nilifanya hivo kisha tukaketi kwenye sofa.


Baada ya mda niliamua kufunguka kuwa nina wasiwasi na mchumba wangu ambaye nataka kufunga naye ndoa huku zikiwa zimebaki siku 3.

Alishangaa kusikia kauli hiyo kwani Rose alikuwa mtu wa Mungu huku akiwa anahamasisha vijana kuwa na mwenendo bora.

Hakuishia hapo lakini pia aliendelea kuniulizia


""Kwa nini huna imani naye"?


Nilitaka kusema kuwa kuna tetesi lakini nikaogopa na kusema basi tu! 

Kauli hiyo hakuielewa kabisa ndipo aliponiambia kuwa huru.

Nilianza kumueleza kuwa kuna habari zimeshasambaa mtaani kuwa anatoka na Baba Paroko.


""Heey...nini...!?"


Sister alishangaa kauli yangu kisha nikamwambia ukweli ndio huo na "tulipokuwa tunakuja kwenye mafunzo, nilikuwa ninasnza mimi kisha yeye  ndo anafuata".

Alichukua rozali yake na maji ya baraka kisha akaniombea na kuniambia kuwa kama ni kweli, Mungu hashindwi chochote.

Nilimuaga kisha nikaondoka nyumbani huku roho yangu ikiwa inauma kwelikweli na kuanza kuwaza itakuwaje kwani siku za kufunga ndoa ndo hizo.

Baada ya kufika nyumbani, mzee alinipa pole na hongera kwa hatua ya mafunzo tuliyofikia huku nikiwa naitikia tu lakini sikuwa na furana.

Nilienda jikoni kisha nikaanza kumueleza mama mwanzo mwisho mpaka mama akawa amebaki ameduwaa.

Mama baada ya taarifa hiyo, aliniambia kuwa " taarifa hizo alikuwa anazisikia mtaani lakini hakutaka kuniambia"


Mhh.."..niliguna kisha mama akaenda kumwambia mzee habari hizo.

Kwa kuwa Mzee wangu alikuwa mwenyekiti wa jumuiya, habari  hizo alizipikea kwa mtizamo hasi.

Alifoka kwelikweli huku akitoa sauti,


"Hee.. ndo mmefikia hatua ya kuwadharirisha watu Mungu aliowapa mamlaka!.. heee!!"

Mzee alisara kwelikweli kama mbogo.

Nilitoka ndani kisha akaanza kumpiga mama.

Nilivyoona hivo,nilirudi ndani ili kumsaidia mama.

Bahati nzuri alifanikiwa kujinasua mikononi mwake.

Mzee alifunga mlango kisha akasema.


"Mlale huko huko na kesho nawapeleka kwenye parokia, kwa udharirishaji!"


Tulikaa nje lakini hakufungua ndipo tulipoenda kulala kwa baba mdogo.

Kesho yake, tulirudi nyumbani, kisha akaniambia niongozane naye mpaka parokiani na kama nisipoenda basi nitakuwa nimejitioa kwenye orodha ya watoto wake.


JE NINI KILIJIRI?..


ITAENDELEANDOA YANGU!

MTUNZI: McLAURIAN

WASAP: 0768276551

PART: 03.

Ilipoishia, tulikaa nje lakini hakufungua ndipo tulipoenda kulala kwa baba mdogo.

Kesho yake, tulirudi nyumbani, kisha akaniambia niongozane naye mpaka parokiani na kama nisipoenda basi nitakuwa nimejitioa kwenye orodha ya watoto wake.

SONGA NAYO..

Baada ya kuambiwa twende parokiani, aisee nilitetemeka sana kwani Paroko alikuwa mtu wa karibu kwangu na hata katika malezi. Hali hiyo ilinifanya nipate wakati mgumu huku zikiea zimebaki siku mbili kabla ya kufunga ndoa.

Mama aliniita na kuniambia kuwa hata kama nitaenda lakini siku ya kufunga ndoa nikatae kabisa mbele ya umati.

Niliguna kisha nikainamisha kichwa.

Baada ya dakika kama kumi hivi, mzee aliniita huku akiwa amevalia kanzu yake nyeupe na kuniambia twende kwa paroko.

Kwa kuwa alikuwa ashanitisha kunitoa nyumbani kwake, sikuwa na namna bali nilikubaliana naye.

Tuliongozana huku njiani akiwa ananiambia,


" Mama yako ndiye anayekupa kiburi subiri sasa, hamuwezi kunidharirisha kwani mie mtu wa heshima. Huyu ni baba yetu wa kiroho na akiamua kukufungia hapa duniani, na mbingunj utafungiwa. Lazima ndoa ifungwe na adhabu juu"


Maneno hayo yaliendelea kunitisha mpaka  nikawa najuta kwanini niliongea maneno hayo .

Hatimaye tulifika kwenye viunga vya kanisa kisha kama bahati hivi, nilikutana na Sister Gaudioza ambaye baada ya kutuona alituita kisha tukamsalimia.

Baada ya hapo, aliniita pembeni kidogo huku akimuomba mzee anisubirie kidogo.

Nilianza kumwambia kuwa mzee kanileta kwa paroko ili aweze kunishitaki kwa maneno ambayo nilimwambia mzee jana.

Sister alishika tama na kisha akanambia kuwa nimuombe Mungu kwani hata Paroko ni Mwanadamu lakini akaniambia niwe makini na ndoa ambayo nakuja kuifunga.


Aliondoka kisha tukaongozana na Mzee mpaka ofisini.

Baada ya kufika ofisini, tulimkuta Katekista kisha akasema Paroko tangu jana usiku hajarudi na anatarajiwa kufika kwenye mida ya saa sita au nne mchana.


Kauli hiyo kwa mbali ilinipa matumaini lakini pia ikaniumiza ba kujiuliza kama aliondoka na Rose ina maana mpaka mda huu yuko naye? na wako wapi mpaka sasa?.


Mzee alimwambia Katekista kuhusu shida yake kama anaweza kuitatua lakini katekista alisema hana mamlaka hayo na ikiwezekana tuendelea kusubiria.

Tulitoka nje kisha mzee akawa ananifokea kwelikweli mpaka Katekista akawa ametuona na kisha akatuita.

Baada ya kuingia ndani, alimuuliza Mzee,


" kulikoni mbona mnarumbana hadharani huku tukiwa maeneo matakatifu"


" Huyu mtoto kashachukua maamuzi ya mama yake na wote wanayofanya nikutaka kuniaibisha na kunidharirisha"


"Sasa mzee mambo ya kifamilia, ongeeni nyumbani muelewane sio kila mtu ajue ya nyumbani kwako"


"Ni kweli lakini hawataki kunisikiliza ninachowambia, sasa ona kesi ambayo wameniletea nyingine"


"Kesi gani tena"?.


"Wanamsingizia Baba Paroko ku...."


"Mhhh...hayo mambo yenu ni makubwa ebu vuteni subira kidogo anakuja mda si mrefu ili muweze kuyaongea mbele yake"


Tulitoka nje kisha nikawa nimekaa pembeni kidogo na mzee maana kila alipokuwa ananiona karibu tu! anaanza kunifokea.

Mda uliendea kusonga mbele mpaka nikawa najihisi  njaa kwelikweli huku nikijisemea kuwa,


" Kama ndoa ni furaha kama wasemavyo mbona kwangu inanitesa hivi wakati hata ndoa yenyewe bado?".


Nilijishika tama huku nikiomba Baba Paroko asiweze kuja kwani  sikujua atanifanyaje maana mzee wangu nilimjua vizuri kwenye kuongea hakuwa na aibu wala hakuwa mtuwa kuficha hata mambo ya familia angeweza kuyamwaga hadharani.


Baada ya kuwa nimewaza, nilitamani kumuomba mzee tuondoke nami niwe tiyari kukubaliana na kila hali na jambo lolote atakalo niambia.

Siku ya kufa nyani, kweli  miti yote huteleza na mbuzi wa maskini kweli hazai.

Nikiwa nimekaa chini ya mti wa kivuli, niliona gari ya Baba paroko huku likiwa speed ya kawaida.

Nilitamani kukimbia lakini gafla mzee naye akaliona gari hilo.

Baada ya kumuona mzee, alishusha kioo kisha wakasalimiana na Mzee nami nikamsalimia.

Aliingia ndani ya geti kisha mzee akaniambia twende ofisini kwa Baba .

Sikuwa na ujanja tena niliona litakalokuwa na liwe kikubwa waniachie uhai wangu. Wakati nawaza hivo niliona kama endapo ataambiwa yote hayo, si anaweza kunichukulia sheria?.

Sikupata majibu huku nikiomba Mzee asiweze kuongea kama kawaida yake.

Baada ya mda kama nusu saa hivi, Paroko alifika ofisini mwake kisha akatukaribisha.

Baada ya ukaribisho mzee aliingia ndani kisha mie nikabaki kwenye benchi ya mapokezi.

Nilitega masikio yangu kisha Mzee akaanza kuongea mwanzo mwisho huku mambo mengine akitia chumvi.

Nilipokuwa sikuamini kama ni mzazi wangu au ni nani maana sio kwa kunikandamiza.

Baada ya kama dakika 10, mzee alitoa kichwa nje kisha akaniita niingie ndani.

Kwa kuwa sikuwa na namna nilifungua mlango kisha nikaingia ndani.

JE NINI KILITOKEA

....ITAENDELEA....
NDOA YANGU!

MTUNZI: McLAURIAN

WASAP: 0768276551

PART: 04.

Ilipoishia, baada ya ukaribisho mzee aliingia ndani kisha mie nikabaki kwenye benchi ya mapokezi.

Nilitega masikio yangu kisha Mzee akaanza kuongea mwanzo mwisho huku mambo mengine akitia chumvi.

Nilipokuwa sikuamini kama ni mzazi wangu au ni nani maana sio kwa kunikandamiza.

Baada ya kama dakika 10, mzee alitoa kichwa nje kisha akaniita niingie ndani.

Kwa kuwa sikuwa na namna nilifungua mlango kisha nikaingia ndani.


SONGA NAYO..


Baada ya kuingia ofisini kwa paroko, nilimkuta Mzee amekaa pembeni yake kisha Paroko akanikaribisha kwenye kiti.

Baada ya ukaribisho huo, alitoa kitabu cha sala na maji ya baraka kisha akaviweka mezani.

Nikiwa ninaogopa nini ataniambia, alinipa kile kitabu na kisha akanambia kurudia maneno ambayo atayasema,


" Ewe baba, ninakiri mbele yako kuwa nimekukosea sana kwa mawazo na kwavitendo. Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie"


Niliitikia maneno hayo kisha akaninyunyuzia maji ya baraka. Baada ya hapo aliniambia kuwa nipo huru na wala hana shida yoyote na mimi.

Mzee alibaki ameshangaa kwani alifikiri kuwa adhabu kali inakwenda kutolewa.


Tuliongozana kisha tukaelekea nyumbani huku mzee akinisihi kutorudia hata siku moja kwani inaonesha picha mbaya kwake.

Baada ya kufika nyumbani, mama aliniita ili kuweza kujua nini kimejiri. Nilimsimulia mwanzo mwisho mpaka mama akawa na furaha.

Jioni yake, ulikuwa mda wa kwenda mafunzo ya mwisho kabla ya kufunga ndoa huku roho yangu ikiwa bado haijapata furaha na kuamini sawasawa.


Baada ya kufika kwenye mafunzo, siku ile Paroko alituita wote kwa pamoja huku akitusihi upendo ili ndoa yetu iweze kudumu.

Wakati anaongea hayo, Rose alionekana mwenye aibu huku 

akiwa anashindwa kumuangalia usoni Baba Paroko.


Kwa kuwa siku ilikuwa imebaki moja, alituruhusu mapema ili tuweze kufanya maandalizi na kisha akatupa mikono ya kila la heri.

Tulitoka nje huku Rose akionekana mwenye aibu fulani tofauti na tulivyokuwa mwanzo.


Hali hiyo ilinifanya niwe na wasiwasi  na kutaka kumuuliza uhusiano wake na Paroko lakini kwa kuwa sikuwa na uthibitisho niliona kunyamaza ili nisilete balaa.

Niliongozana naye barabarani kisha tukapita kwenye kundi la wanawake waliokuwa wamesimama barabarani, baada ya kupita nilimsikia mmoja akisema,


"Huyo ndo anatembea na Paroko"


Kwa kuwa nilikuwa na Rose pembeni, nilijifanya sijasikia chochote huku nikianzisha mada nyingine kwani niliona aibu kwa kauli ile.


Tuliagana kisha kila mtu akaenda nyumbani kwao.

Nikiwa naelekea nyumbani, nilianza kuamini kuwa lisemwalo lipo na kama halipo laja kwani haiwezekani kila kona ni yeye tu.

Nilijipa msimamo kuwa sitokuwa tiyari kufunga naye ndoa hata kama watanilazimisha.


Miongoni mwa wanakwaya wenzangu, alinipigia kuwa kuna sintofahamu kati ya Rose na Paroko kwani kuna mtu aliwaona wakiwa wanakunywa bia huku mazingira yakiwa sio rafiki kabisa.


Kauli hiyo iliendelea kunichanganya kabisa..

Baada ya kufika nyumbani, mzee alikuwa tiyari ashaandaa kondoo mmoja na beberu mmoja aliyekuwa amenona kwelikweli  huku akidai kuwa wageni rasmi watakula kuku ambao tulikuwa nao nyumbani.


Nilienda kumwambia mama kuwa kila sehemu ninapopita naona wanatoa habari ya Rose. 

Mama alinisihi kukataa kufunga ndoa kwani sitokuwa na amani maishani mwangu.


Mawazo hayo niliyachukua lakini mzee nilimjua  vizuri kabisa na nikawaza kama  nikikataa je na hivi vitu itakuwaje?.

Hatimaye siku iliyokuwa imesubiriwa ikawadia huku nikiwa na mawazo kwelikweli.

Nilivaa suti yangu kisha na shahidi wangu wa ndoa pamoja na ndugu jamaa na marafiki.


Tulipofika kanisani, tuliwakuta upande wa bibi harusi wakiwa na furaha kwelikweli huku Rose akiwa anafanana kama malaika mpaka  nikajiuliza ndo huyu au naona vibaya?.

Baada ya mda tuliingia kanisani kwa ajili ya zoezi husika.

Nilipofika kanisani, nilihisi kama kitu fulani hivi kinavuta nafsi yangu mpaka nikawa naonekana kuwa kuna jambo moyoni.


Baba Paroko alianza ibada kisha akatoa utaratibu kuwa katikati ya ibada ndipo atakapofungisha pingu ya maisha.

Niliposikia neno hilo, nilitamani kutoa machozi lakini kwa kuwa  nilikuwa kwenye umati wa watu, nikawa najilazimisha kuonesha furaha.

Hatua yenyewe ilitimia kisha tukanyanyuka kuelekea Alutare huku vifijo na nderemo vikitawala kwelikweli.

Baba Paroko alitunyunyuzia maji ya baraka kisha kutwambia kurudia maneno ambayo atatwambia na kisha kujibu ndio au hapana.

Baada ya kumaliza kauli hiyo, niliona kama mwanga fulani machoni mwangu kisha akatoweka.

Baba Paroko alianza kazi yake,


" Bi Rosemary unamkubali bwana David kuwa mme wako wa ndoa kwa hali yoyote, magonjwa na furaha?.


" Ndio ninakubali"


"Bwana Devid unamkubali Bi Rosemary kuwa mke wako wa ndoa kwa hali yoyote , magonjwa na furaha"?.


""Mmmm....ndio../ Hapana"


"Narudia tena Bwana Devid unamkubali Bi Rosemary kuwa mke wako wa ndoa kwa hali yoyote , magonjwa na furaha"?.


"Mmhh.....HAPANA, HAPANA, HAPANA"


Baada ya kauli hiyo ya kukataa katakata huku  nikiwa na ujasiri, waumini wote waliangua kicheko huku Rose akibaki na amesimama.


JE  NINI KILIJIRI?...


         TAENDELEA  .....

NDOA YANGU!

MTUNZI: McLAURIAN

WASAP: 0768   276   551

PART: 05

Ilipoishia, Baada ya kauli hiyo ya kukataa katakata huku  nikiwa na ujasiri, waumini wote waliangua kicheko huku Rose akibaki na amesimama.

SONGA NAYO...

Baada ya kukataa, nilirudi kwenye benchi kukaa huku waumini wakiwa wanaunguruma kwelikweli.

Watu hawakuamini lakini ukweli ubaki kuwa palepale.

Paroko aliendelea na ibada kama kawaida na ibada ilipoisha tukatoka nje.

Baada ya kufika nje, Mzee alinifuata akataka kunigombeza lakini walimkamata na kumwambia twende nyumbani tukayaongee.

Kwa upande wa Rose nao hawakuamini huku akiwa amevalia shera yake.

Waliendelea kuimba kama kawaida huku nikawa naona mpaka aibu.

Tulipofika nyumbani, tulikuta chakula tiyari huku watu wakiwa wamesubiria bwana harusi na bibi harusi.

Walishangaa kutuona tupo peke etu huku mzee akiwa anapiga kelele kwelikweli.

Baada ya mda walipata kizima kisha kila mtu akastaajabu kwani wengi wao hawajawahi kuona wala kusikia.

Kwa kuwa chakula kilikuwa tiyari, watu walikula na kunywa huku nikiwa sina amani kabisa.

Wakati tupo nyumbani, kumbe Rose na wapambe wake walikuja kijijino kwetu kisha Rose akafichwa kwa Baba mdogo.

Kesho yake, Mzee aliitisha kikao cha wanaukoo kisha wakaanza kulijadili hili suala.

Waliamua na kusema kuwa lazima nifunge naye ndoa kwani ni kitendo cha aibu ambacho kinadharirisha familia na ukoo kwa ujumla.

Sikuweza kukubaliana lakini waliendelea kusema kuwa kama nitaendelea kukataa, watanifuta kwenye ukoo na hata familia.

Sikutoa majibu ya moja kwa moja siku hiyo lakini  niliona bora kukubaliana na hali kwani wazee wote walionekana kuchukizwa kwelikweli.

Kesho yake, Mzee alirudi kwa Baba paroko kisha akamwambia kuwa nimekubali hivo mchakato uendelee.

Baba Paroko alimwambia kuwa hakuna haja ya kuja tena kanisani na badala yake tuanze mafunzo upya ambayo yatatolewa na katekista nyumbani.

Katekista alianza kutoa mafunzo kwa baba mdogo ambapo ndipo Rose alipokuwa amehifadhiwa.

Mafunzo hayo yalichukua takribani mwezi mmoja na nusu kabla ya ndoa kufungwa.

Baada ya mda huo kukamilika, Baba paroko alikuja nyumbani mida ya saa kumi na moja jioni ili kuweza kutufungisha ndoa.

Rose alisindikizwa na wapambe na mashahidi wake kisha nami nikawa na mashahidi wangu.

Baada ya kumsogelea karibu Roose, niliona tumbo likiwa limechomoza na kuleta kiashiria cha moja kwa moja kuwa tiyari ana mimba.

Nikiwa nashangaa, gafla nilianza kuona akina mama wanasoge pembeni huku wakiwa wamebana vicheko kwelikweli.

Nilianza kujihisi uchungu mkubwa huku nikiwa namatumaini ya kuwa sijawahi kutana naye kimwili labda angesema hiyo mimba ni ya kwangu.

Mama alinimonyeza kwa macho lakini sikuwa na ujanja wowote.

Baba Paroko alitufungisha ndoa kisha nikaamua kukubali lakini moyo wangu kamwe haukufurahia.

Wapambe wa Rose walishangilia na kisha Paroko akamalizia kwa kusema,


" kilichounganishwa na Mungu, mwanadamu asikitenganishe .milele""


Kauli hiyo iliniuma kwelikweli kisha Paroko akaondoka.

Majirani wa karibu walianza kumiminika nyumbani na kuanza kutoa mkono wa pongezi kwa bibi harusi na bwana harusi.

Wakati naendelea kuwa na masikitiko ya kimoyomoyo huku uso na sura yangu vikinitahidi kuonesha furaha, niliamua kutulia kwani ushatokea lakini nikahisi tumbo hilo ni kitambi.

Ilipofika usiku, shangazi alienda chumbani kwangu kisha akatandika mashuka meupe kwelikweli.

Mila zetu kila ukioa, unawekewa shuka jeupe afu baada ya ufunguzi shuka hilo hurudishwa kama ushahidi kwa familia ya binti aliyeolewa na ndipo hupongezwa kwa malezi bora.

Baada ya mda shangazi alituita pamoja na Rose kisha akaondoka na kunambia nisiwaangushe.

Nilicheka kwelikweli.

Rose alianza kuvua shela yake ili asiichafue huku nikiwa na hamu kwelikweli ya kujua kama tumbo hilo ni la kitambi au mimba.

Wakati anafanya hivo, nami nilianza kuvua suti yangu kisha nikabakiza bukta na vesti .

Baada ya kutoa shela, alibaki na kisketi kifupi na blauzi kisha nikamvuta kidogo nakuanza kumpapasa.

JE NINI KILIFUATA?

ITAENDELEA 

Bofya HAPA Lipia tsh 1000 Tu kwa mtandao wowote

Uimalizie    
  
Unaweza pia kupenda

Maoni Andika maoni